S H E I K H

l o a d i n g
shia taqiya

SHIA NA TAQIYA

Taqiya, ni neno la kiarabu ambalo linatafsiriwa kama 'kinga' katika lugha ya kiswahili. Katika maneno mengine, ni kusema kwamba unaficha uhalisia fulani ili usidhurika.Taqiya imekuwa ikifanyika tangu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Wakati ambapo Uislamu ulikuwa katika hali ya uchanga, ili wabidi Waislamu wafundishane katika hali ya kujificha, walikuwa wakifanya hivi kujiepusha na madhara ambayo wangeyapata kutoka kwa maquraish wa Makkah. Kuna visa vingi tu vya maswahaba ambao iliwabidi wakubaliane na batili na kuicha haki huku wakiendelea kuamini katika haki ili kulinda usalama wao.


Hata hivyo, kwa muda sasa pamekuwa pakitengenezwa tuhuma dhidi ya Waislamu wa madhahebu ya Shia Ithna-Asheri kwamba wao sio Waislamu (wanafanya taqiya) ni wanafiki.


Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kuandika kitabu 'Shia na Taqiya' akijibu na kutolea hoja juu ya suala hili na kubainisha msimamo wa Mashia juu ya habari ya taqiya.

  • Jun 28, 2024
khitma maiti abdilahinassir

JE, KHITMA INAMFIKIA MAITI? | SEHEMU #1 | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Katika jamii za Kiislamu kumekuwa na maswali juu ya habari za usomaji wa khitma!


Je, historia inasema nini kuhusu habari za khitma? | Je, kuna umuhimu gani wa kusoma khitma | Je khitma inamfikia maiiti? | Kwa nini kumekuwa na ikhtilafu juu ya habari za khitma?


Haya ni miongoni mwa maswali ambayo marhoum sheikh Abdilahi Nassir ameyatolea hoja...

  • Jun 07, 2024
khitma maiti abdilahinassir

JE, KHITMA INAMFIKIA MAITI? | SEHEMU #2 | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Katika jamii za Kiislamu kumekuwa na maswali juu ya habari za usomaji wa khitma!


Je, historia inasema nini kuhusu habari za khitma? | Je, kuna umuhimu gani wa kusoma khitma | Je khitma inamfikia maiiti? | Kwa nini kumekuwa na ikhtilafu juu ya habari za khitma?


Haya ni miongoni mwa maswali ambayo marhoum sheikh Abdilahi Nassir ameyatolea hoja...

  • Jun 07, 2024
wasia mirathi abdilahinassir

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA WASIA | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Habari za wasia ni miongoni mwa mambo muhimu kwani pamoja na mambo mengine zinagusa eneo la mirathi ambapo aghalabu (suala la mirathi) limekuwa lenye kusumbua miongoni mwa jamii za Kiislamu. Je, Uislamu unalitazama vipi suala la wasia?


Sheikh Abdilahi Nassir (r.a) alitoa hoja juu ya suala hili.


  • Jun 08, 2024
maulid bidaa haramu

JE, MAULID NI BIDA'A? | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Kumekuwa na utamaduni wa muda mrefu kwa jamii za Kiislamu kufanya hafla za Maulid au Sherehe za mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Aghalabu sherehe hizo huwajumuisha waislamu bila kujali tofauti zao za kiitikadi na kumsifu Mtume kwa namna mbalimbali.


Hata hivyo, katika jamii hizo za Kiislamu kumekuwa na mtazamo mseto juu ya uendeshaji wa maulid hizo. Wapo katika Waislamu wanaosema kuwa Maulid ni bida'a na hata kufikia kuiharamisha lakini pia wapo ambao wanatilia mkazo juu ya uendeshaji wa hafla hizo na kila undi likiwa na hoja zake.


Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kutoa hoja zake juu ya suala hili lakini pia kuangazia nafasi ya sherehe za maulid kwenye jamii za Kiislamu...

  • Jun 28, 2024