SHIA NA HADITHI
Hadithi, ni moja kati ya mambo muhimu ambayo yanatoa muongozo kwenye mambo mbalimbali ndani ya Uislamu.
Hata hivyo, kumekuwa na tuhuma zimekuwa zikielekezwa kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia Ithana-Asheri juu ya kuwa na mtazamo tofauti juu ya namna wanavyozitazama hadithi.
Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kuandika kitabu 'Shia na Hadithi' akijibu na kutolea hoja juu ya suala hili.
- Jun 28, 2024
SHIA NA QURAN
Uislamu unaundwa na viungo kadhaa, miongoni mwavyo ni kuamini kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah (S.W.T) na Muhammad (s.a.w.w) ni mtume wake mwisho miongoni mwa mitume walioagizwa kutulingania.
Hata hivyo, ni jambo la wazi kwamba sasa Uislamu umegawanyika kiitikadi hususani kwenye eneo la uongozi baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Hali imepelekea kila kundi katika Uislamu kujiona kuwa ni sahihi zaidi kuliko lingine na ndani yake kukatokea kushutumiana kwenye mambo mbalimbali. Kwa mfano, kumekuwa na hoja kutoka upande mmoja ukidai kwamba wafuasi wa Maimamu 12 (Shia Ithna-Asheri) wana Qur'an (msahafu) wao tofauti na unaotumiwa na jamii nyingine za Kiislamu.
Je, hoja hiyo ina ukweli kiasi gani?, Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kuandika kitabu 'Shia na Qur'an' akijibu na kutolea hoja juu ya suala hili.
- Jun 28, 2024
SHIA NA TAQIYA
Taqiya, ni neno la kiarabu ambalo linatafsiriwa kama 'kinga' katika lugha ya kiswahili. Katika maneno mengine, ni kusema kwamba unaficha uhalisia fulani ili usidhurika.Taqiya imekuwa ikifanyika tangu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Wakati ambapo Uislamu ulikuwa katika hali ya uchanga, ili wabidi Waislamu wafundishane katika hali ya kujificha, walikuwa wakifanya hivi kujiepusha na madhara ambayo wangeyapata kutoka kwa maquraish wa Makkah. Kuna visa vingi tu vya maswahaba ambao iliwabidi wakubaliane na batili na kuicha haki huku wakiendelea kuamini katika haki ili kulinda usalama wao.
Hata hivyo, kwa muda sasa pamekuwa pakitengenezwa tuhuma dhidi ya Waislamu wa madhahebu ya Shia Ithna-Asheri kwamba wao sio Waislamu (wanafanya taqiya) ni wanafiki.
Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kuandika kitabu 'Shia na Taqiya' akijibu na kutolea hoja juu ya suala hili na kubainisha msimamo wa Mashia juu ya habari ya taqiya.
- Jun 28, 2024