S H E I K H

l o a d i n g
maulid bidaa haramu

JE, MAULID NI BIDA'A? | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Kumekuwa na utamaduni wa muda mrefu kwa jamii za Kiislamu kufanya hafla za Maulid au Sherehe za mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Aghalabu sherehe hizo huwajumuisha waislamu bila kujali tofauti zao za kiitikadi na kumsifu Mtume kwa namna mbalimbali.


Hata hivyo, katika jamii hizo za Kiislamu kumekuwa na mtazamo mseto juu ya uendeshaji wa maulid hizo. Wapo katika Waislamu wanaosema kuwa Maulid ni bida'a na hata kufikia kuiharamisha lakini pia wapo ambao wanatilia mkazo juu ya uendeshaji wa hafla hizo na kila undi likiwa na hoja zake.


Sheikh Abdilahi Nassir alipata fursa ya kutoa hoja zake juu ya suala hili lakini pia kuangazia nafasi ya sherehe za maulid kwenye jamii za Kiislamu...

  • Jun 28, 2024
hija makkah

MAANA YA HIJA | SHEIKH ABDILAHI NASSIR

Ibada yaHija ni moja ya nguzo muhimu katika Uislamu ambapo, kila Muislamu anatarajiwa kuhiji angalau mara moja katika maisha yake ikiwa ana uwezo.


Hata hivyo, uzoefu unaonesha kumekuwa na mitazamo tofauti juu ya namna watu wanavyoichukulia ibada hiyo. Kwa mfano, wapo wanaichukulia ibada hiyo katika mtazamo wa kiroho tu lakini pia wapo ambao wanaitazama ibada ya hija kama fursa ya kupitisha na kuendesha ajenda nyingine kwa maslahi mapana ya Uislamu...


Sheikh Abdilahi Nassir, alitoa hoja zake juu ya namna watu hususani Waislamu wanavyopaswa kuichukulia ibada ya hija.

  • Jun 28, 2024
wasia mirathi abdilahinassir

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA WASIA | SHEIKH ABDILAHI NASSIR.

Habari za wasia ni miongoni mwa mambo muhimu kwani pamoja na mambo mengine zinagusa eneo la mirathi ambapo aghalabu (suala la mirathi) limekuwa lenye kusumbua miongoni mwa jamii za Kiislamu. Je, Uislamu unalitazama vipi suala la wasia?


Sheikh Abdilahi Nassir (r.a) alitoa hoja juu ya suala hili.


  • Jun 08, 2024