S H E I K H

l o a d i n g

Article

HAWLI YA MARHOUM SHEIKH ABDILAHI NASSIR | 2023


Uongozi wa Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ukiongozwa na mwenyekiti wake Haj Hussein Karim, umeshiriki kikamilifu kwenye hawli ya marhoum Sheikh Abdillahi Nassir iliyofanyika March 5, 2023 katika ukumbi wa Delh Dabar – Upanga, jijini Dar es salaam.


Wengine kutoka BMMT walioshiriki kwenye hawli hiyo ni pamoja na Haj Abdul wahid Mohammed – Makamo Mwenyekiti, na Sheikh Msabaha Mapinda – Mkuu wa Idara ya Tabligh BMMT.


Viongozi wengine kutoka taasisi mbalimbali walihudhuria katika hawli hiyo akiwemo Haj Amine Nassor – mwenyekiti wa Africa Federation (AFED) aliyeambatana an makamo wake, Haj Aunali Khalfan. Wengine ni Imam wa masjid Khoja Dar es salaam - Syed Adeel Raza aliyeambatana na Haj Anwar Dharamsi - Mwenyekiti mstaafu wa AFED.


Vilevile hawli hiyo ilihudhuriwa na kiongozi wa Jumuiya ya Shia Ithana Asheri Tanzania – Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Stambuli Nassir (mtoto wa Sheikh Abdillahi Nassir), Sheikh Jabir Chandoo, Sheikh (Dkt). Abdul razaq Amir na wageni wengine waalikwa.

 

Wazungumzaji walipata fursa ya kueleza namna walivyomtambua marhoum Sheikh Abdillahi Nassir vilevile kuangalia mchango wake katika harakati za kitablighi na kujenga umoja baina ya waislamu bila kujali tofauti zao za kiitikadi/madhehebu.


Sheikh Abdillahi Nassir alifariki Jan 11, 2021 nyumbani kwao nchni Kenya na amefanya kazi nyingi zikiwemo za uandishi wa vitabu mbalimbali kama vile Shia na Hadithi, Shia na Qur-an, Shia na Taqiya, Maulid Si Bidaa Si Haram na vingine vingi ambavyo vinatolewa bure kwenye duka la vitabu la Bilal lililopo ofisi kuu mtaa wa Libya, karibu na kituo cha mwendokasi Kisutu, Dar es salaam au kwenye tovuti ya taasisi www.bilal.or.tz au tovuti maalumu www.sheikh.co.tz